Simu murwa ya Infinix Hot S3 hatimaye imewasili Tanzania. Ni habari nzuri sana ukizingatia kuwa simu hii bado haijafika Kenya.
Hot S3 inasifika sana kwa sababu ya kamera yake kali pamoja na kioo kilicho na muundo wa kisasa.
Sifa zake ndizo hizi.
Kioo
Upana wa Kioo: 5.7-inch
Aina ya Kioo: IPS LCD
Resoluti: 720×1440 Pixels
Umakini wa Resoluti: 282 ppo
Kioo cha Hot S3 ni moja ya sababu kuu ya wewe kununua kifaa hichi. Kioo ni kipana na kina design ya kisasa ya 18:9.
Hii yamaanisha kuwa kama wewe una uraibu wa kutazama video na kucheza gemu kwa simu, Infinix Hot S3 yakufaa.
Design
Saizi: 152.30 x 72.80 x 8.40
Uzani: 150g
Infinix Hot S3 ina design time sana. Wembamba wake utaupenda. Hot S3 ina uzani wa gramu mia na hamsini peke kwa hivyo ni rahisi kuibeba.
CPU na mengineyo
Uendeshaji: Android 8.1
Processor: 1.4GHz octa-core
Saizi ya RAM: 3 GB
Ukubwa wa Memory: 32GB
Memori kadi: Yes, up to 128 GB
Infinix walifanya kazi nzuri sana na CPU ya Hot S3. Sii hii yakupa processor aina 1.4GHz octa-core. Processor hii ina mbio sana. Gemu nzito na applications zacheza vyema kwa hii simu.
Kamera
Kamera ya nyuma: 13 MP
Kamera ya mbele: 20 MO
Flashi: Ndio
Kamera ndio sababu kuu yakufanya ununue Hot S3. Hii simu yakupa camera ya saizi 20 MP ya kuchukua selfie!
Hii ni pamoja na kamera kali ya 13MP ya kuchukua picha.
Battery
Uwezo wa battery: 4000 mAh
Infinix Hot S3 ina battery yenye uwezo ya 4000 mAh. Hii ya maanisha kuwa waeza itumia hii kwa hadi siku mbili bila ya kuichaji sana sana kama utumizi wako ni wa wastani.
Bei Bora Tanzania
Je wataka kununua Hot S3? Simu hii ina bei ya TSh 489,000 huku Tanzania. Jumia wana offer, ukinunua Hot S3, utapata zawadi ya memori kadi.
Waionaje Infinix Hot S3, tupe maoni yako!
Kevin is a tech enthusiast and the lead writer at MobiTrends.co.ke. He has been writing about smartphones and tech related topics since October 2012. About Us | Contact Us